• HABARI MPYA

    Monday, August 31, 2020

    HAMAD HILIKA ASAJILIWA MTIBWA SUGAR NA KUFUNGA MABAO MAWILI KATIKA USHINDI WA 6-2 LEO GAIRO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kumsajili mshambuliaji Ibrahim Hamad Ahmada 'Hilika' kutoka Zimamoto ya Zanzibar.
    Hilika anacheza nafasi ya ushambuliaji, mfungaji bora mara mbili ligi kuu Zanzibar msimu 2019/2020 na 2016/2017, Pia amewahi kuibuka mfungaji bora katika kombe la Mapinduzi Cup.
    Hilika almaarufu striker wa nchi amesaini mkataba wa miaka miwili kukitumikia kikosi cha wana tam tam.

    Mtibwa Sugar imemsajili mshambuliaji Ibrahim Hamad 'Hilika' kutoka Zimamoto ya Zanzibar 

    Hilika pia ni mchezaji tegemeo katika kikosi cha Zanzibar Heroes, Huu ni usajili wetu wa nane na mwisho kuelekea msimu wa 2020/2021.
    Wengine wapya Mtibwa Sugar ni Abubakar Ame Omar AbalKassim Khamis, Baraka Gamba Majogoro, George Makanga, Geofrey Luseke na Hassan Kessy Ramadhan.
    Wakati huo huo: Mtibwa Sugar imeibuka na ushindi wa 6-2 dhidi Kombaini ya Gairo katika mchezo kirafiki Uwanja wa CCM Gairo. 
    Mabao ya Mtibwa Sugar leo yamefungwa na Boban Zirintusa, Ibrahim Hilika mawili kila mmoja na Abdul Haule moja.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HAMAD HILIKA ASAJILIWA MTIBWA SUGAR NA KUFUNGA MABAO MAWILI KATIKA USHINDI WA 6-2 LEO GAIRO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top