• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 28, 2020

  MTIBWA SUGAR YAFANYA MABADILIKO MADOGO KATIKA BENCHI LAKE LA UFUNDI, BARNABAS AULA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Mtibwa Sugar ya Morogoro imefanya mabadiliko madogo katika benchi lake la ufundi kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzana Bara.
  Zubery Rashid Katwila ataendelea kuwa Kocha Mkuu, lakini amebadilishwa wasaidizi na kuanzia sasa Msadizi wake namba moja atakuwa Vincent Barnabas Saramba.
  Awali, Barnabas alikuwa kocha mkuu timu za vijana ambaye alipata mafanikio makubwa akiwa na timu hizo za vijana kwa kutwaa ubingwa wa taifa wa vijana chini ya umri wa miaka 20 na kuzalisha wachezaji wengi waliopandishwa timu ya kwanza.

  Kutoka kulia; Vincent Barnabas, Zubery Katwila na Awadh Juma 

  Aidha, mabadiliko mengine yamehusu nafasi ya kocha wa makipa, Soud Slim ambaye kama Katwila na Barnabas ni mchezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar – amechukua nafasi ya Patrick Mwangata.
  Awadh Juma Issa ‘Maniche’ ndiye kocha mpya wa timu za vijana za Mtibwa Sugar, ingawa atakuwa chini ya Barnabas ambaye ataendelea kuwa kocha mkuu wa timu hizo pamoja na majukumu yake mapya.
  Akiwa mchezaji wa nafasi ya kiungo, Awadh Juma amekitumikia kikosi cha Mtibwa Sugar kwa mafanikio makubwa kabla ya kustaafu msimu uliopita tu.
  Wengine wanaounda Benchi la Ufundi la Mtibwa Sugar ni Daktari; Lawrence Mushi, Msimamizi wa vifaa vya timu; Amir Abdallah na Meneja wa timu, David Chitty Bugoya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAFANYA MABADILIKO MADOGO KATIKA BENCHI LAKE LA UFUNDI, BARNABAS AULA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top