• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 28, 2020

  PARIMATCH TANZANIA YAINGIA MKATABA WA MWAKA MMOJA KUIDHAMINI MBEYA CITY LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMPUNI ya Parimatch Tanzania imesaini mkataba wa mwaka mmoja kuidhamini klabu ya Mbeya City ambayo inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara. 
  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utawala wa kampun ya Parimatch Tanzania, Tumaini Maligana amesema kwamba wameingia rasmi makubaliano ya mkataba wa udhamini wa Mbeya City kwa msimu wa 2020/2021.
  TAARIFA KAMILI YA PARIMATCH;
  “Habari za Asubuhi, Kwa majina naitwa Tumaini Maligana Ni Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utawala wa Parimatch Tanzania.Ningependa kuchukua fursa hii kuwakaribisha katika hafla yetu ya kutambulisha rasmi udhamini wetu kwa Klabu ya Mbeya City ambayo inashiriki michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara. 

  Kwanza nichukue fursa hii kupongeza uongonzi na wachezaji wote wa mbeya city kwa kuendelea kushiriki ligi kuu Tanzania bara .
  Tunatambua Uwepo - ( Waandishi kutoka media mbalimbali, Ndugu waalikwa kutoka maeneo tofauti tofauti)
  Nianze kuizungumzia Parimatch: Kampuni yetu Parimatch inaendesha shughuli michezo ya kubashiri mtandaoni na imesajiliwa na bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania kwa takriban miaka 3 sasa. Kimataifa tupo zaidi ya nchi 15 ikiwa na wateja zaidi ya milioni moja duniani kote.
  Ndani ya hii miaka mitatu tumeendesha programu mbalimbali za kuinua michezo Tanzania kama Amsha ndoto na leo ni hatua nyingine tunapiga katika kukuza michezo.
  Tunapenda kuutaarifu umma kuwa Leo IJUMAA Tar 28 August 2020  tumeingia rasmi makubaliano ya mkataba wa udhamini wa Klabu ya Jiji la Mbeya ‘Mbeya City’, ambayo inashiriki michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara katika msimu huu wa 2020/2021.
  Mkataba huu ni wenye faida pande zote mbili. Mbeya City ni moja klabu kubwa kwa hapa Tanzania hususani ukiangalia idadi ya mashabiki na ushawishi katika soka. 

  Sisi kama Parimatch Moja ya jukumu letu kubwa ni kuhakikisha michezo inakua kuanzia ngazi ya chini hadi ngazi ya kimataifa. Lakini pia Tunaendelea na michakato mablimbali ya kuunga mkono vilabu vingine kutoka ligi kuu ,  ligi daraja la kwanza na hata Vilabu Chipukizi . Ikiwa ni kuunga mkono juhudi za TFF na bodi ya ligi kuhakikisha ligi za Tanzania zinakuwa na tunaenda kimataifa.
  Hivyo umeamua kuunga mkono mbeya city , ili wapenzi wasoka waendelee kupata burudani stahiki . 
  Kwa kumalizia: EPL : ( uwezekano fadili ligi kuu )
  Promotion ( bega kwa bega na mashabiki wa klabu na wapenzi wa soka )  zawadi mbalimbali . 
  Elimu (Responsible ) - Jinsi ya kushinda
  Tovuti , Mitandao ya kijamii , Habari kedekede ( bonasi Mbalimbali )
  Jackpot - Jackpot rahisi sana - (shilingi 100 , Mechi 10 tu na kushinda Milioni 10 ) hii ni rahisi sana . 
  Mwisho , niwashuuru sana wadau wote wa soka nchini , kuanzia TFF , Bodi ya Michezo , Mbeya City - kuwa kutupokea kuwa wadau rasmi wa michezo Ahsanteni Sana,”.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PARIMATCH TANZANIA YAINGIA MKATABA WA MWAKA MMOJA KUIDHAMINI MBEYA CITY LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top