• HABARI MPYA

    Thursday, August 20, 2020

    KIUNGO MZIMBABWE NEVER TIGERE AONGEZA MKATABA WA MIAKA MIWILI AZAM FC

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO nyota, Mzimbabwe Never Tigere amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kendelea na kazi katika klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam.
    Mkataba huo utamfanya kuendelea kusalia kwa wababe hao wa Chamazi hadi mwaka 2022.
    Tigere amekuwa na kiwango kizuri msimu uliopita, akisajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili akitokea Platinum ya Zimbabwe, na kufanikiwa kufunga mabao manne katika Ligi Kuun ya Tanzania Bara, mawili kati ya hayo akitupia kwa mikwaju ya adhabu ndogo, na kuchangia pasi mbili.
    Wakati huo hu: Timu ya Azam FC itatambulisha kikosi chake cha msimu ujao kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo FC Jumapili kwenye Tamasha la Azam FC Festival Uwanja wa Azam Complex.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIUNGO MZIMBABWE NEVER TIGERE AONGEZA MKATABA WA MIAKA MIWILI AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top