• HABARI MPYA

  Jumatatu, Agosti 17, 2020

  LIGI KUU TANZANA BARA KUANZA KUTIMUA VUMBI SEPTEMBA 6, SIMBA NA YANGA KUUMANA OKTOBA 18

  LIGI Kuu ya Tanzania Bara inatarajiwa kuanza Septemba 6, mwaka huu, mabingwa watetezi, Simba SC wakifungua dimba na Ihefu FC Uwanja wa Uwanja wa High Land Estate, Mbarali mkoani Mbeya.
  Watani wao wa jadi, Yanga SC wataanzia nyumbani, Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya.
  Mechi nyingine zote za ufunguzi zitatanguliwa na mechi ya Ngao ya Jamii Agosti 29 kati ya mabingwa wa Kombe ka Shirikisho la Soka Tanzana (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation (ASFC) Namungo FC na mabingwa wa Lig Kuu Smba SC Jumapaili ya Saa 11:,00 Uwanja wa Mkapa.
  Wenyewe kwa wenyewe, watani wa jadi, Yanga na Srmba watakutana Oktoba 18 katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIGI KUU TANZANA BARA KUANZA KUTIMUA VUMBI SEPTEMBA 6, SIMBA NA YANGA KUUMANA OKTOBA 18 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top