• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 26, 2020

  MATUNDA YA TAMASHA, KINDA WA CHAMAZI KOMBAINI ACHUKULIWA AKADEMI YA AZAM FC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KUPITIA michuano ya Wiki ya Chamazi iliyohitimishwa kwa kilele cha Tamasha la Azam FC Festival, klabu hiyo imefanikiwa kupata mchezaji mmoja atakayeingia moja moja kwenye kituo chake cha vjana, maarufu kama Azam FC Academy.
  Kijana huyo ni kiungo mshambuliaji, Haji Sultan Kambangwa, aliyekuwa akichezea Chamazi Combine, iliyoibuka bingwa wa michuano hiyo kwa kuichapa Ngawina S.A bao 1-0.
  Mchango wa Tamasha la Azam FC Festival, umeanza kuonekana ikiwa ni mara ya kwanza tu kufanyika, tunawaomba Wakazi wa Chamazi muendelee kujivunia, timu yenu ya nyumbani ya Azam FC.

  Wakati huo huo: Tawi la mashabiki wa Azam FC mkoani Mwanza, lilitumia siku ya kilele cha Tamasha la Azam FC Festival, kutembelea kituo cha watoto yatima cha Kilimahewa mjini humo na kutoa misaada mbalimbali.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MATUNDA YA TAMASHA, KINDA WA CHAMAZI KOMBAINI ACHUKULIWA AKADEMI YA AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top