• HABARI MPYA

  Jumatatu, Agosti 31, 2020

  MTIBWA SUGAR YASAJILI WENGINE WAWILI JUMA NYANGI NA ABUBAKAR AME NA KUFIKISHA SABA WAPYA JUMLA


  KLABU ya Mtibwa Sugar imemsajili kiungo wa kati Juma Nyangi Ganabali kutoka Alliance FC ya Mwanza iliyoshuka daraja kwa mkataba wa miaka miwili. 

  Mtibwa Sugar imemsajili beki, Abubakar Ame Omar kutoka Malindi FC ya Zanzibar ambaye pia yumo kwenye kikosi cha timu ya visiwani humo, Zanzibar Heroes akiwa anamudu kucheza nafasi za beki wa kati, kiungo wa chini na beki wa kulia.
  Pichani kutoka kushoto ni Mohamed Jabr (Mwenyekiti Malindi), Swabr Abubakar (Ofisa wa sheria na utawala Mtibwa Sc), Abubakar Ame, Mohamed Masoud (Katibu Malindi) na Hussein Ahmada (meneja wa mchezaji)
  Sasa Mtibwa Sugar imesajili wachezaji wapya saba, wengine AbalKassim Khamis, Baraka Gamba Majogoro, George Makanga, Geofrey Luseke na Hassan Kessy Ramadhan.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YASAJILI WENGINE WAWILI JUMA NYANGI NA ABUBAKAR AME NA KUFIKISHA SABA WAPYA JUMLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top