• HABARI MPYA

    Sunday, August 16, 2020

    YANGA WAKIENDA CAS WATASHINDA RUFAA KESI DHIDI YA MORRISON

    Na Mwikwabi James, DAR ES SALAAM
    NIMEOYAONA Mashtaka ya Bernad Morrison dhidi ya Yanga kuhusu Mkataba wake, Lakini pia nimeona hukumu iliyotolewa na Kamati ya sheria na hadhi ya wachezaji katika kesi husika...

    MASHTAKA YA MORRISON;
    Bernad Morrison, Malalamiko yake yalikuwa kwanza kwenye Utofauti wa Tarehe ya Mchezaji husika (Morrison) Kusaini na Tarehe ambayo Mkataba husika ulisajiliwa kwenye Mfumo wa TMS ya FIFA
    Malalamiko ya pili ni kukatwa maandishi kwenye moja ya kurasa ya Mkataba husika NB (KUKATWA KWA KUTUMIA PENI) Na siyo kukwata kwa mkasi au kuchanwa kwa mikono

    HUKUMU ILIYOTELWA NA YAKAMATI YA SHERIA NA HADHI YA WACHEZAJI YA TFF
    Kwanza kamati ilitambua kuwepo mkataba kati ya Yanga na Bernad Morrison, Lakini pia  Kamati ilimpa ushindi Bernad Morrison kwasababu kuna dosari waliziona kwenye mkataba husika....Hivyo basi Bernad Morrison akawa huru kwa kusema kuwa hana Mkataba na Klabu ya Yanga kutokana na Dosari ambazo kamati ilizibaini.

    SHERIA INASEMAJE SASA?
    Sheria inasema, kuwepo dosari kwenye Mkataba hakuwezi kuvunja mkataba wala haiwezi kusababisha mkataba kutokuwepo. kwasababu Kuna dosari ambazo kisheria zinaweza kurekebishika  kisheria tunaita CURABLE....Dosari ambazo zilijitokeza kwenye Mkataba wa Morrison na Yanga ni Curable...Utofauti wa Tarehe ni Curable yani inaweza kurekebishika, lakini pia dosari zingine zote nazo zipo kwenye kundi la Curable

    VITU GANI VINAWEZA KUSABABISHA MKATABA KUTOKUWEPO
    Wakati nafanya Degree ya Human Resource Management (HRM) Mwalimu wangu wa labor law, Mr Mgabuso, Alitufundisha vitu viwili vinaweza kuvunja mkataba na kufanya mkataba kutotambulika,
    Mambo hayo mawili yanayoweza kusababisha mkataba kuvunjika na kutokuwepo ni kama yafuatayo
    (1) IF THERE IS NO CONSIDERATION
    (2) IF THERE IS NO FREE CONSENT

    NO CONSIDERATION:
    Kwenye Consideration, ni pale mnapokubaliana, Tunakuajili au Tunakupa mkataba wa miaka miwili alafu Kampuni au taasisi husika inasema itakuwa inakulipa kiasi fulani cha Pesa.....Sasa kama Kampuni au Taasisi husika ikashindwa kukupa malipo husika, hapo tunasema hakuna Consideration hivyo basi automaticaly kuna breach of Contract au Kuvunjika kwa Mkataba na kufanya Mkataba kutokuwepo Tena....Kwa kesi hii ya Morrison Bernad hakukuwa na Malalamiko yote kutoka kwa Morrison Bernad yanayosema HAKUWAHI KULIPWA MALIPO WALIYOKUBALIANA KWENYE MKATABA NA YANGA..

    (2) CONSENT
    Kwenye Consent, Mkataba unaweza kuvunjika au kutokuwepo kama upande mmoja umeingia kwenye mkataba kwa kulazimishwa.

    VIASILI VYA CONSENT
    (1) Unsound mind/ Sound Mind
    Unsound mind ni mtu ambaye  haruhusiwi kuingia Mkataba na mtu, Kampuni au Taasisi yeyote. Watu ambao wapo katika Unsound mind ni Mwendawazimu/ Chizi, Watu hawa ukiingia nao mkataba kisheria mkataba husika automaticaly unakuwa haupo...Kwasababu Sheria inakataza kuingia mikataba na Unsound people.....
    Swali, Je? Bernad Morrison ni Unsound Person? 

    KUNDI LA PILI NI 
    Minor age, Kundi hili linawahusisha watu wenye umri chini ya Miaka 18, Sheria inakataza Mtu, Taasisi au kampuni yeyote kuingia Mikataba na Mtu mwenye miaka chini ya 18, na Sheria inasema ukiingia mkataba na Mtu mwenye umri chini ya Miaka 18 Mkataba huo unakuwa hautambuliki na haupo.....Swali, Je? Bernad Morrison ana Umri Chini ya miaka 18?

    KIPENGELE CHA MWISHO KINACHOWEZA KUSABABISHA MKATABA KUTOKUWEPO NI..
    Kisheria tunaita COERCION
    Coercion, Means the action or practice of peronaling someone to do something by using force or threats... Kwa tafasiri isiyo rasmi, ni kitendo chakumlazimisha mtu kufanya tendo fulani kwa nguvu.....Kisheria Mtu akilazimishwa kusaini mkataba kwa nguvu haidha kwa kushikiwa bunduki, Mapanga au Kwa vitisho vya Maneno basi mkataba husika unakuwa haupo ata kama alisaini.....Swali, Je? Bernad Morrison kuna sehemu yeyote amewahi kusema alilazimishwa kusaini kwa nguvu mkataba husika haidha kwa Kushikiwa Bunduki, Mapanga, au Kwa vitisho vya Maneno ana kwa ana au kwa njia ya Simu?

    MAJIBU NI HAPANA...
    Kwa kuangalia msingi wa hukumu iliyotolewa na Kamati ya Sheria na hadhi ya Wachezaji kwa kumpa Ushindi Bernad Morrison juu ya Dosari ambazo zilikuwepo kwenye Mkataba ambazo ni CURABLE yaani zinarekebishika, Sababu ambazo haziwezi kusababisha kutokuwepo kwa Mkataba, Kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji haijaitendea Haki Klabu ya Yanga....Bernad Morrison ana Mkataba halali na Klabu yake ya Yanga, Ila mkataba una dosari ambazo wanaweza kukaa pande mbili yaani Bernad Morrison mwenyewe pamoja na Klabu yake ya Yanga wakazirekebisha...

    YANGA WAENDE CAS, KESI HII USHINDI UPO KWAO......NA CAS NINA HAKIKA WATAWASHANGAA WANASHERIA WALIOTOA HUKUMU HII, WATABAKI WANAJIULIZA WANAIJUA KWELI SHERIA? AU PESA ILIPITISHWA ILI SHERIA IPINDISHWE...
    (Mwikwabi James 'Legendary' anapatkana kwa namba ya smu +255 766 074 160)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA WAKIENDA CAS WATASHINDA RUFAA KESI DHIDI YA MORRISON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top