• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 15, 2020

  MAMBO MAZURI KESHO UZINDUZI WA WIKI YA CHAMAZI UWANJA WA AZAM COMPLEX, TAMASHA BABU KUBWA LA MASHABIKI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Azam FC kesho Jumapili asubuhi itaifungua Wiki ya Chamazi Uwanja wa Azam Complex, itakayohitimishwa kwa Tamasha kubwa la Azam FC Festival Agosti 23 mwaka huu.
  Wiki ya Chamazi itaanza kwa mbio za Jogging mapema asubuhi zitakazomalizikia uwanjani Azam Complex kabla zoezi rasmi la ufunguzi kufanyika saa 4.00 asubuhi.
  Mara baada ya ufunguzi huo kutakuwa na mechi za vyombo mbalimbali vya habari, zitakazofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex.
  Tamasha la Azam FC Festival ni kwa ajili ya mashabiki wote wa wa timu hiyo na wa soka kwa ujumla kutoka sehemu mbalimbali nchini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAMBO MAZURI KESHO UZINDUZI WA WIKI YA CHAMAZI UWANJA WA AZAM COMPLEX, TAMASHA BABU KUBWA LA MASHABIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top