• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 26, 2020

  SIMBA SC YACHEZA MECHI MBILI KWA MPIGO LEO ASUBUHI YASHINDA ZOTE, YAIPIGA KMC 3-1 NA TRANS CAMP 5-2 UHURU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KATIKA kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii, Simba SC wamecheza mechi mbili za kirafiki leo asubuhi Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Mechi ya kwanza wameibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya KMC na ya pili wameshinda 5-2 dhidi ya Transit Camp ya daraja la kwanza, zote za Dar es Salaam,.
  Dhidi ya KMC mabao ya Simba yamefungwa na Clatous Chama dakika ya 28, Ibrahim Ajibu dakika ya 33 na Muzamil Yassin dakika ya 57.
  Dhidi ya Trans Camp mabao ya Simba SC yamefungwa na Cyprian Kipenye mawili, Charles Ilamfya, Meddie Kagere na Gardiel Michael.

  Ngao ya Jamii ni mechi ambayo hukutanisha bingwa wa Ligi Kuu, Simba SC na washindi wa Azam Sports Federation Cup, Namungo FC – kuashiria upenuzi wa pazia la msimu mpya itachezwa Jumapili kuanzia Saa 9:30 Alasiri Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YACHEZA MECHI MBILI KWA MPIGO LEO ASUBUHI YASHINDA ZOTE, YAIPIGA KMC 3-1 NA TRANS CAMP 5-2 UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top