• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 03, 2020

  MECHI YA WATANI WA JADI YENYE UTANI WENYE UTANI NDANI YAKE

  Na Mustafa Mtupa, DAR ES SALAAM
  NIKIWA napambana na ugonjwa wa usingizi katika asubuhi moja wapo ambapo sauti ya jogoo ilinifanya nigundue kuwa Mda wa kupona ugonjwa huo umeshawadia hivyo ni wajibu wangu kufungua macho yangu yaliyojawa na uzito usio kifani ,sauti ya simu yangu ya mkononi ikapenya vyema masikioni mwangu kuashiria kuna mtu alikuwa anahitaji kusikia sauti yangu kwakuwa alikuwa anapiga.
  Kiuvivu niliinyanyua simu hiyo na kutazama namba ambayo ilikuwa inapigwa niligundua kuwa namba hiyo ni Ngeni kabisa kwakuwa ilikuwa haina Jina  kabisa.
  Niliitazama sekunde kadhaa kabla ya kuipokea.baada ya kuipokea nilikuatana na sauti nyembamba iliyopita bila kupingwa,wala kukwama kwama masikioni mwangu kwa jinsi ilivyokuwa nyembamba.
  Ilikuwa ni simu ya mwanadada ambaye alianza kwa kusifia kazi yangu ya uandishi wa Makala na kunitaka niendelee kukaza buti.Zilikuwa ni simu za kawaida lakini pia za thamani sana kwangu kutoka kwa wadau wangu lakini kwa siku hiyo ilikuwa tofauti kidogo kwakuwa ilikuwa ni simu ya mwanamke maana mara zote nilizowahi kupigiwa zilikuwa ni simu za wanaume.
  Nikimshukuru mwanadada huyu na mwisho akanikumbusha kuwa kwenye makala iliyopita niliahidi hapa kuwa nitakuaja na makala kuhusu Mechi hii ya kesho hivyo nisisahau kuandika maana anahitaji saana mtazamo wangu kuhusu hili huku akininambia kuwa yeye alikuwa shabiki wa simba na simba ikishinda basi nimtafute ana soda yangu bariidi.
  Baada ya simu ile nikajikuta naingiwa na shauku ya kutaka kuiongelea mechi hii kwa kuandika jambo kwenye ukurasa huu.kwangu naiangalia hii mechi kwa vitu vifuatavyo.

  ➕USAILI WA WACHEZAJI WAPYA UNAWEZA UKAPOOZESHA MECHI AMA UKACHANGAMSHA.

  kivipi usajili huo unaweza kuleta ushindanj au kupoozesha mechi.

  Kwa kawaida timu zoote zimesajili wachezaji ambao kwa kiasi kikubwa wanatazamiwa kuonyesha kitu kupitia mechi hii ya Tarehe nne jambo ambalo kwangu naiona sio Afya kwa Wachezaji hawa.kwasababu watakuwa wanacheza kwa presha kubwa.
  Kawaida mchezaji akiwa kwenye hali hii ya kuwa anamulikwa saana na ukizingatia na ukubwa wa mechi husika.kuna baaadhi ya wachezaji wanaweza kupambana na  hali hii kutokana na ukomavu wao.lakini kuna wachezaji hushindwa kupambana na  hali hii.
  Kuna baadhi ya wachezaji wakiwa katika hali hii huwa wanahitaji kuonesha kitu kikubwa zaidi  ya kile ambacho wanacho mwisho wa siku wanajikuta wanatoka Nje ya kile mwalimi alichofundisha na pia wanajikuta wanakosea saana kwakuwa watajilazimisha kutoa zaidi ya uwezo wao. kitu ambacho kitaufanya mchezo huu kupooza kwakuwa kila mchezaji atacheza kwa maoni yake na sio maoni ya kocha.
  Ikiwa wachezaji hawa watajaribu kusahau kwamba wanacheza moja ya Derby kubwa Afrika na kucheza kama wanavyocheza kila siku.huku macho yao yakiwa kwenye mikono ya makocha wao nikiw ana maana wakiangalia maelekezo ya makocha zao hao basi ni wazi kuwa mchezo huu utakuwa ni wa kuchangamka na tutashuhudia mbungi la aina yake.japo hili huitaji wachezaji ambao wana ukomavu wa kiakili ili kucheza chini ya presha.
  Nakumbuka nyakati za kwanza naanza kufanya matangazo  ya mpira mwalimu kashasha alinambia niitoe taswira kwamba nasikilizwa na watanzania million 50 na nifanye kama natangaza na sisikilizwi hii itanisaidia kuondoa presha niliyokuwa nayo.

   ➕KUTAKUWA NA ART OF DIFFENDING
  Jambo la kuongeezea kwenye mechi hii ni suala la sanaa ya uzuiaji.
  Kwangu naiona ni mechi ambayo inakutanisha safu Ngome mbili za uzuiaji zinazofanya vizuri kwa sasa.
  Uwepo wa mabeki wa kati wenye height ya kutosha pamojaa na uwepo wa namba sita wenye uwezo mzuri zaidi wa kunusa hatari ni jambo ambalo linaashiria mechi hii kuwa na ukame wa magoli.Makame, Feisal na Banka kwa upande wa yanga katika eneo la kati kati huku Fraga,Mkude na mzamiru kwa upande wa simba ni viungo ambao wana utashi mzuri zaidi kwenye kuzuia jambo linalo nifanya nione ugumu kwenye mechi hii.
  Huku katika maeneo ya mabeki wa kati Lamine,Yondani ama Sonso ni mabeki walio kwenye pic kwa sasa. 
  Huku simba Wawa,Tairone,Kennedy na Mlipili pia ni mabeki ambao wapo kwenye pic yao kwa sasa.
  La kuongezea hapa ni kuwa hamasa pia ni jambo muhimu sana ambalo litatufanya tushuhudie mchezo wa ushindani sana Determination ya wachaji itakuwa ya juu sana kama kutakuwa na hamasa ya kutosha kuanzia ya kifedha na hamasa ya mashabikj uwanjani.
  Yote kwa yote ni mechi ngumu saana lakini kwangu inaweza ikaamuliwa zaidi na pointi ya kwanza niliyo iweka hapo juu.
  By the way huu ni mtazamo wangu.tukutane taifa,wale watakao hitaji kuniiona wanitafute nitakuwa hapo.😁😁😁
  Nisaidie kuniwish maana leo nasheherekea kumbu kumbu ya siku yangu ya kuzaliwa,kama unakeki napokea.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MECHI YA WATANI WA JADI YENYE UTANI WENYE UTANI NDANI YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top