• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 03, 2020

  STARTIMES YAPATA KIBALI CHA KUONYESHA 'EMIRATES FA CUP'

  Na Saada Akida, DAR ES SALAAM
  KAMPUNI ya Startimes wameanza mwaka 2020 kwa kishindo baada ya kupata kibari cha kurusha mechi za kombe la FA maarufu kama 'Emirates FA Cup' moja kwa moja kutoka England.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Startimes, David Malisa amesema kwamba kampuni hiyo imepokea kibali hicho cha mwaka mmoja kuanzia 2020 hadi 2021 na mechi hizo zitatangazwa kwa  lugha zote.
  Alisema michezo huyo itaanza kurushwa kuanzia kesho (Januari 4) huku Jumapili wakendelea kuonyesha michezo mingine kupitia channel zao za michezo.
  "Startimes imewafikia watanzania kuwa wanatambua wapenzi wa soka, hivyo wanaboresha na kuleta burudani za soka," alisema Malisa.
  Alisema katika Kuhakikisha na kuboresha channel za mpira watakuwa na Euro 2020, Copa Italia na Bundasliga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: STARTIMES YAPATA KIBALI CHA KUONYESHA 'EMIRATES FA CUP' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top