• HABARI MPYA

  Tuesday, September 05, 2017

  JOSHUA KUTETEA MATAJI YAKE YA IBF, WBA NA WBC OKTOBA 28

  BONDIA Anthony Joshua amethibitisha atatetea mataji ya ngumi za kulipwa uzito wa juu duniani ya vyama ya IBF, WBA na IBO kwa kupigana na Kubrat Pulev mjini Cardif, Oktoba 28.
  Muingereza huyo aliunganisha mataji hayo baada ya kumpiga Wladimir Klitschko Uwanja wa Wembley Aprili 29, mwaka huu na amesema hawezi kuchelewa kumvaa Mbulgaria huyo kutetea taji lake.
  Joshua amethibitisha kuwepo kwa pambano hilo baada ya Pulev kutangaza Jumatatu kwamba watapigana Uwanja wa Principality mjini Cardif, Oktoba. 
  Anthony Joshua amethibitisha atatetea mataji ya ngumi ya IBF, WBA na IBO dhidi ya Kubrat Pulev mjini Cardif, Oktoba 28

  Joshua alitakiwa kuhakikisha anatetea anatetea taji lake la IBF kwa kupigana na mshindani namba moja, Pulev kabla ya Desemba 2 au kujihatarisha kuvuliwa taji hilo.
  Lakini pambano hilo la Cardiff, ambalo linaweza kufanyika kwenye Uwanja wenye paa la kufunga wa Principality ni moja ya mapambano ambayo Joshua anayafurahia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JOSHUA KUTETEA MATAJI YAKE YA IBF, WBA NA WBC OKTOBA 28 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top