// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); DOLE HILI LOTE ANANYOOSHEWA NANI, REFA MFARANSA...AU? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE DOLE HILI LOTE ANANYOOSHEWA NANI, REFA MFARANSA...AU? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Tuesday, September 05, 2017

  DOLE HILI LOTE ANANYOOSHEWA NANI, REFA MFARANSA...AU?

  MSHAMBULIAJI chipukizi wa England, Dele Alli yuko hatarini kufungiwa baada ya kuonyesha alama ya dole la kati katika ushindi wa England wa 2-1 dhidi ya Slovakia Uwanja wa Wembley usiku wa jana.
  Ilionekana kama Alli anamuonyeshea dole hilo refa Mfaransa, Clement Turpin, lakini nyota huyo wa Tottenham akasema baada ya mechi kwamba alikuwa anataniana na mchezaji mwenzake wa England, Kyle Walker.
  Alli ameomba radhi kupitia akaunti yake ya Twitter: "Ni kufafanua, alama ya dole usiku huu ilikuwa utani baina yangu rafiki yangu mzuri Kyle Walker! Naomba radhi kwa usumbufu wowote niliosababisha!' 
  Dele Alli yuko hatarini kufungiwa baada ya kuonyesha dole la kati jana England ikimenyana na Slovakia Uwanja wa Wembley

  Picha za TV kwa mwonekano mzuri Uwanja wa Wembley zinaungana na utetezi wake.
  Lakini FIFA wakigundua alimlenga refa Turpin, Alli atakuwa hatarini kufungiwa kuanzia mechi tatu, zikiwemo mbili za mwisho za kufuzu dhidi ya Slovenia na Lithuania na ya kwanza ya Fainali zijazo za Kombe la Dunia England ikifuzu.
  Mwezi June, Muargentina Lionel Messi alifungiwa mechi nne kwa kumtukana mshika kibendera, kuonyesha kiasi gani FIFA hawana mzaha juu ya utovu wa nidhamu kwenye mchezo.
  Kocha wa England, Gareth Southgate amesema: "Sikuona, lakini ninajua hilo. Kyle na Dele walikuwa wanataniana, na Dele alinyoosha dole kuelekea kwa Kyle. Sifahamu ilikuwa eneo gani la uwanjani. Wawili hao wamekuwa wana namna yao ya kuwasiliana, lakini hivyo ndivyo walivyosema suala hilo lilipoibika,"..
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DOLE HILI LOTE ANANYOOSHEWA NANI, REFA MFARANSA...AU? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top