// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AS KIGALI YAMCHUKUA SHABIKI WA RAYON KWA OFA NZURI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AS KIGALI YAMCHUKUA SHABIKI WA RAYON KWA OFA NZURI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Monday, September 04, 2017

  AS KIGALI YAMCHUKUA SHABIKI WA RAYON KWA OFA NZURI

  Na Canisius Kagabo, KIGALI 
  TIMU ya AS Kigali ya Rwanda, imemnunua shabiki maarufu wa mahasimu wao wa Jiji, Rayon Sports aitwaye Rwarutabura.
  Na hayo yanatokea siku chache baada ya AS Kigali kuwachukulia Rayon kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Nshuti Dominique Savio aliyeondoka The Blues kuhamia kwa ‘Wana Mji’.
  AS Kigali imejiimarisha kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Azam Rwanda kwa kumajili Savio aliyekuwa anachezea kwa wapinzani wao wa Jiji Kigali, Rayon Sports.
  Rwarutabura alikuwa shabiki maarufu wa Rayon Sports  
  Lakini kwa sasa ni shabiki wa Wana Mji wa Kigali

  Baada ya pigo la uwanjani, mabingwa wa Ligi Kuu ya Azam Rwanda wamepata pigo la jukwaani pia, kufuatia Rwarutabura kuachana na The Blues kwenda kwa ‘Wana Mji’.
  Rwarutabura ni shabiki mzoefu na maarufu hata Afrika Mashariki kutokana na staili za ushabiki wake na amedumu Rayon Sports kwa miaka mingi iliyopita, lakini sasa hivi ameamua kuvua rangi za bluu na nyeupe na kuvaa njano na kijani.
  Akizungumuza na Bin Zubeiry Sports – Online jana, Rwarutabura alisema kwamba yeye anaipenda Rayon Sports, lakini baada ya kupewa ofa nzuri na AS Kigali imebidi abadilishe maisha.
  “Rayon Sports naipenda sana, tangu nikijua mambo ya soka ni Rayon Sports tu, lakini mambo yamebadilika kazi ni kazi. Ushabiki wangu nimeshajua unaweza kubadilisha maisha yangu na familia yangu ndiyo sababu inanifanya niachane na Rayon Sports kwa sababu AS Kigali itanilipa mshahara na imenunulia nyumba ina maana, nitaachana na kulipa kodi,”alisema Rwarutabura 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AS KIGALI YAMCHUKUA SHABIKI WA RAYON KWA OFA NZURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top