• HABARI MPYA

  Sunday, July 02, 2023

  WAZIRI WA MICHEZO AGAWA VIFAA VYA MICHEZO NJOMBE


  WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, ambaye pia ni Mbunge wa Mkoa wa Njombe (Viti Maalum), amekabidhi vifaa vya michezo ikiwemo mipira pamoja na mabati 152 katika Shule ya Sekondari Madilu iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe.
  Mhe. Chana amekabidhi vifaa hivyo Julai 1, 2023 shuleni hapo ambapo amewasitiza wanafunzi wa shule hiyo kusoma kwa bidii, kuongeza nidhamu pamoja na kuonesha vipaji vyao katika Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuwa ni miongoni mwa sekta zenye fursa ya ajira kwa sasa.
  "Masuala ya Utamaduni, Sanaa na Michezo lazima yapewe kipaumbele, kila shule inayosajiliwa lazima kuwe na miundombinu ya michezo ambapo katika shule 56 za michezo zilizotengwa zikiwemo Matola na Makambako za Mkoa wa Njombe ni miongoni mwa shule zitakazokarabatiwa kwa ajili ya kukuza michezo, amesema Mhe. Chana
  Ameongeza kuwa, katika mwaka huu wa fedha wizara itatekeleza Programu ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mtaa kwa Mtaa ambapo amesisitiza jamii kutobadilisha matumizi maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya michezo pamoja na kuyalinda.
  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mhe. Victoria Mwanziva amewataka wazazi kusimamia wanafunzi wa shule hiyo na nyingine kuhudhuria masomo, pamoja na kushiriki shughuli za maendeleo katika wilaya hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAZIRI WA MICHEZO AGAWA VIFAA VYA MICHEZO NJOMBE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top