• HABARI MPYA

  Sunday, July 30, 2023

  SIMBA SC YASHINDA 4-1 MECHI YA KIRAFIKI KAMBINI UTURUKI


  TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya timu ya Batman Petrolspor katika mchezo wa kirafiki kwenye kambi yake ya kujiandaa na msimu mjini Ankara nchini Uturuki.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Soğuksu Spor Kompleksi, mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji Mcameroon, Willy Essomba Onana, kiungo Mrundi Saido Ntibanzokiza, beki Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na mshambuliaji na Nahodha John Raphael Bocco.
  Huo ulikuwa mchezo wa nne kwa Simba katika kambi yake ya kujiandaa na msimu nchini Uturuki, baada ya Alhamisi kucheza mechi mbili na Turan FK ya Turkmenistan na kushinda 2-0 kabla ya kufungwa 1-0, wakati mechi nyingine walitoa sare ya 1-1 na Zira FK ya  Azerbaijan Julai 24.
  Batman Petrolspor ni timu inayoshiriki Lig 3 ambayo ni ngazi ya nne katika mfumo wa ligi za Uturuki, baada ya Süper Lig, Lig 1 na Lig 2 na mafanikio yake makubwa kihistoria ni kucheza Lig 2 pekee.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YASHINDA 4-1 MECHI YA KIRAFIKI KAMBINI UTURUKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top