• HABARI MPYA

    Thursday, July 27, 2023

    SIMBA SC YACHAPWA 1-0 NA TURAN FK LEO UTURUKI


    KLABU ya Simba imepoteza mechi ya Kwanza katika kambi yake ya kujiandaa na msimu mjini Ankara nchini Uturuki baada ya kuchapwa 1-0 na Turan FK ya Turkmenistan, bao la dakika ya nne la Roderik Miller jioni ya leo.
    Huo ulikuwa mchezo wa marudiano baina ya timu hizo baada ya mchana wa leo Simba kushinda 2-0, mabao ya Kibu Dennis na Nahodha, John Raphael Bocco.
    Kwa ujumla Simba imekwishacheza mechi nne kwenye kambi yake ya kujiandaa na msimu nchini Uturuki baada ya sare ya 1-1 na Zira FK ya  Azerbaijan Julai 24.
    Turkmenistan ni nchi inayopatikana Asia ya Kati ikiwa imepakana na Kazakhstan upande wa Kaskazini Magharibi na Uzbekistan kwa Kaskazini Mashariki, ambayo kwa sasa inashika nafasi ya 138 kwenye renki za FIFA ikiwa chini ya Tanzania ambayo ipo nafasi ya 123.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YACHAPWA 1-0 NA TURAN FK LEO UTURUKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top