• HABARI MPYA

  Saturday, July 29, 2023

  YANGA YASHINDA 10-0 MECHI YA KIRAFIKI KIGAMBONI LEO


  MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 10-0 dhidi ya timu ya Magereza katika nchezo wa kirafiki kwenye kambi yake ya kujiandaa na msimu huko Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga leo yamefungwa na Kennedy Musonda na Clement Mzize kila mmoja matatu, Pacôme Zouzoua, Skudu Mahlatsi Makudubela, Stephane Aziz Ki na Maxi Mpia Nzengeli.
  Huo ni mchezo wa pili tu wa kujipima kwa Yanga baada ya Julai 22 kuibuka na ushindi wa 1-0, bao la Musonda dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YASHINDA 10-0 MECHI YA KIRAFIKI KIGAMBONI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top