• HABARI MPYA

    Friday, July 28, 2023

    NAIBU WAZIRI MWANA FA AKUTANA NA MWAKILISHI WA LA LIGA KUZUNGUMZIA SOKA YA VIJANA


    NAIBU Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ amekutana na kufanya mazungumzo na mwakilishi wa La Liga nchini Tanzania, Jorge Gazapo kwa ajili ya kuangalia maeneo mbalimbali wanayoweza kushirikiana na wizara katika kuendeleza sekta ya michezo hapa nchini.
    Mhe. Mwinjuma amekutana na mwakilishi huyo  leo Julai  27 2023 jijini Dar es salaam ambapo katika mazungumzo hayo,  wamekubaliana kuendeleza soka la vijana kwa La Liga kuweka makambi kila mwaka kwa watoto wenye umri wa miaka 10 mpaka 18 na makocha 50.
    Pamoja na hayo wamekubaliana La Liga kuaandaa mafunzo ya ujuzi kwa watoto ambayo yatafanyikiwa  ESC Laliga nchini Spain,  aidha watoto wenye vipaji  watachaguliwa kwa makundi ya chini ya miaka 14 na wengine chini ya miaka 17 na watasafirishwa kwenda Spain kwa ajili ya mafunzo zaidi.
    Mhe.  Mwinjuma amemuahidi Mwakilishi wa La Liga nchini Tanzania kumpa ushirikiano wote utakaohitajika ili kufanikisha azma hiyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NAIBU WAZIRI MWANA FA AKUTANA NA MWAKILISHI WA LA LIGA KUZUNGUMZIA SOKA YA VIJANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top