• HABARI MPYA

  Friday, July 21, 2023

  MISS TANZANIA 2023 KUONDOKA NA BENZ NA SH MILIONI 10 LEO MASAKI


  WAREMBO 20 wabaki vinywa wazi mara baada ya kutangazwa rasmi zawadi ya Miss Tanzania   gari aina ya Mercedes benz yenye thamani ya Shilingi Milioni 30 za Kitanzania pamoja na pesa taslim  Milioni 10 kwa atakaeibuka Mshindi Usiku wa Leo  katika ukumbi wa Superdome Masaki Jijini Dar es salaam. 
  Akizungumza na Wanahabari wakati wa kutambulisha zawadi hiyo. Jijini Dar es salaam Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa, amesema kuwa Fainali ya Miss Tanzania  itapambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa warembo wenyewe huku akisisitiza kuwa Fainali hiyo itakuwa ya kitofauti kutokana na kupangika kwa matukio ya kiburudani zaidi.
  "Nilipata nafasi ya kupita kambini kushuhudia mazoezi ya Fainali ya Miss Tanzania kutoka kwa washiriki wenyewe Kiukweli kuna hatari watu wanajifua namna ya kutembea jukwaani (catwalk) zaidi ya Mrembo Halima Kopwe (Miss Tanzania 2021) lipieni ving'amuzi mshuhudie burudani hiyo kupitia chaneli ya  St bongo ndani ya Startimes. "
  Malisa amewasihi watazamaji kulipia mapema ving'amuzi vyao ili kutazama mubashara Fainali hizo kwa wale ambao hawatabahatika kufika katika ukumbi wa the Superdome Masaki Jijini Dar es salaam. 
   Nae Meneja Mradi wa shindano hilo Ombeni Phiri amesema Washiriki hao  20 kutoka  kanda mbalimbali wanaenda kugombania gari hiyo ambapo ni kwa mara ya pili mfululizo gari aina ya Mercedes benz kutolewa kwa mshindi.
  "Warembo 20 wamekuwa kambi kwa siku 27 na kujifunza vitu mbalimbali hivyo sio jambo rahisi kwa warembo hao  kuwa sehemu moja kutokana na kila mshiriki ana tabia yake.''
  Hata hivyo Phiri amewatakia kila la heri warembo hao 20 kuelekea fainali hiyo ambapo mmojawapo anaenda kubadilisha maisha yake kupitia tasnia ya urembo na mitindo. 

  Hata hivyo kwa upande Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Azam Mashango amesema washiriki wote 20 watapewa fedha kama kiinua mgongo isipokuwa  Mshindi wa nne,tano na sita  watapewa Milioni 1 ,Mshindi wa 3 milioni 2 huku Mshindi wa pili akipatiwa Milioni 2 na wa kwanza milioni 10 huku Mshindi wa 6 hadi 20 wakiambulia laki 2 kila mmoja. 
  Mashango amewapongeza wadau mbalimbali wa shindano hilo wakiwemo Robby One pharmacy, Startimes na wengine  kuhakikisha shindano hilo linafanyika na linaonyeshwa mubashara kwenye King'amuzi hicho ili kuwapa nafasi wadau wa urembo kuwaona wasichana hao wadogo wenye kiu ya kutimiza ndoto zao kupitia tasnia ya urembo. 
  ORODHA YA WASHINDI WA TAJI LA MISS TANZANIA
  2023 Halima Kopwe
  2022 Juliana Rugumisa
  2019 Sylvia Sebastian
  2018 Queen Elizabeth Makune
  2017 Julitha Kabete
  2016 Diana Edward Lukumay
  2015 Lilian Kamazima
  2014 Happiness Watimanywa
  2013 Brigitte Alfred Lyimo
  2012 Lisa Jensen
  2011 Salha Kifai
  2010 Genevieve Emmanuel Mpangala
  2009 Miriam Gerald Unplaced
  2008 Nasreen Karim
  2007 Richa Adhia
  2006 Wema Sepetu
  2005 Nancy Sumari
  2004 Faraja Kotta
  2003 Sylvia Bahame
  2002 Angela Damas
  2001 Happiness Magese
  2000 Jacqueline Ntuyabaliwe
  1999 Hoyce Temu
  1998 Basila Mwanukuzi
  1997 Saida Kessy
  1996 Shose Sinare
  1995 Emily Adolf
  1994 Aina Maeda
  1967 Theresa Shayo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MISS TANZANIA 2023 KUONDOKA NA BENZ NA SH MILIONI 10 LEO MASAKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top