• HABARI MPYA

  Monday, July 17, 2023

  MBWANA SAMATTA AHAMIA PAOK FC YA UGIRIKI  NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amejiunga na klabu ya Paok FC ya Ugiriki kutoka Fenerbahçe ya Uturuki baada ya misimu miwili ya kucheza kwa mkopo Ubelgiji.
  Samatta aliyeibukia African Lyon mwaka 2008 kabla ya kwenda Simba 2010 ambayo ilimuuza TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mwaka 2011.
  Alicheza Mazembe kwa mafanikio hadi mwaka 2016 alipouzwa KRC Genk ya Ubelgiji ambako pia Januari mwaka 2020 aliuzwa Aston Villa ya England ambako Septemba alitolewa kwa mkopo Fenerbahçe.
  Julai mwaka 2021 akasaini mkataba wa miaka minne kujiunga moja kwa moja na Fenerbahçe ambako pia mambo hayakumuendea vizuri akapelekwa kwa mkopo Ubelgiji, kwanza Royal Antwerp mwaka 2021 na baadaye akarejea Genk kuanzia 2022.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBWANA SAMATTA AHAMIA PAOK FC YA UGIRIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top