• HABARI MPYA

    Friday, July 14, 2023

    YANGA SC YATAMBULISHA BEKI MPYA KUTOKA ASEC MIMOSAS


    KLABU ya Yanga imemtambulisha beki wa kulia, Kouassi Attohoula Yao (26) kuwa mchezaji wake mpya wa tano kutoka  ASEC Mimosas ya kwao, Ivory Coast.
    Wachezaji wengine wapya wa kigeni Yanga ni winga Maxi Mpia Nzengeli kutoka Maniema ya kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na beki wa kati Gift Freddy kutoka SC Villa ya kwao, Uganda.
    Yanga pia imesajili wazawa wawili, beki wa kushoto Nickson Kibabage kutoka Singida Fountain Gate na kiungo Jonás Mkude kutoka kwa mahasimu, Simba SC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YATAMBULISHA BEKI MPYA KUTOKA ASEC MIMOSAS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top