• HABARI MPYA

  Monday, July 17, 2023

  KOUAME ALIVYORIPOTI KAMBINI SIMBA SC UTURUKI LEO


  WINGA wa kushoto, Aubin Kramo Kouamé aliyesajiliwa kutoka ASEC Mimosas ya kwao, Ivory Coast leo ameripoti kwenye kambi ya Simba mjini Ankara nchini Uturuki kwa maandalizi ya msimu mpya.
  Aubin Kramo Kouamé ni mmoja kati ya wachezaji wapya watano waliosajiliwa Simba SC, wengine ni beki mzawa, David Kameta ‘Duchu’ kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, beki wa katí Che Fondoh Malone Junior kutoka Cotton Sport ya kwao, Cameroon, kiungo Mkongo Fabrice Luamba Ngoma kutoka Al Hilal ya Sudan na mshambuliaji Mcameroon, Leandre Essomba Willy Onana kutoka Rayon Sport ya Rwanda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOUAME ALIVYORIPOTI KAMBINI SIMBA SC UTURUKI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top