// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WAZIRI WA MICHEZO APOKEA VIFAA KWA AJILI YA SAMIA TAIFA CUP NA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WAZIRI WA MICHEZO APOKEA VIFAA KWA AJILI YA SAMIA TAIFA CUP NA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, July 11, 2023

    WAZIRI WA MICHEZO APOKEA VIFAA KWA AJILI YA SAMIA TAIFA CUP NA


    WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dk. Pindi Chana jana amepokea vifaa vya michezo kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Chen Mingjian Jijini Dar es Salaam ambavyo vitatumika katika Programu ya Michezo Mtaa kwa Mtaa pamoja na Samia Taifa Cup.
    Vifaa mbavyo Mhe. Chana amepokea ni pamoja na Mipira ya Kikapu 600, mipira ya Wavu 600, mipira ya Miguu 600 pamoja na Jezi 2634.
    "Vifaa hivi tutavikabidhi katika mikoa yetu yote Tanzania Bara na Zanzibar bila kusahau Shule zetu mbili za michezo kwa kila Mkoa, naamini vifaa hivi vitanuafaisha vijana wetu katika kukuza vipaji ambavyo vitawasaidia wao binafsi na Taifa letu" amesema Mhe. Chana.
    Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Chen Mingjian amesema nchi yake inaendelea kushirikiana na Tanzania katika Sekta mbalimbali ikiwemo kubadilishana uzoefu wa wataalamu na ujenzi wa miundombinu ya michezo nchini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAZIRI WA MICHEZO APOKEA VIFAA KWA AJILI YA SAMIA TAIFA CUP NA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top