• HABARI MPYA

  Sunday, July 09, 2023

  CHE MALONE FONDOH NI MCHEZAJI MPYA WA TATU SIMBA SC


  KLABU ya Simba imemtambulisha beki wa katí, Che Fondoh Malone Junior kuwa mchezaji wake mpya kwa mkataba wa miaka miwili kutoka Coton Sport ya kwao, Cameroon.
  Che Fondoh Malone Junior (24), anakuwa mchezaji mpya wa tatu tu Simba SC baada ya winga wa kushoto, Aubin Kramo Kouamé kutoka ASEC Mimosas ya kwao, Ivory Coast na mshambuliaji Mcameroon, Leandre Essomba Willy Onana kutoka Rayon Sport ya Rwanda.
  Malone anatua Msimbazi baada ya kuisaidia Coton kilichotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Cameroon huku yeye mwenyewe akishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu wa 2022-2023.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHE MALONE FONDOH NI MCHEZAJI MPYA WA TATU SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top