• HABARI MPYA

  Thursday, July 13, 2023

  SIMBA SC YAPUUZIA SEMINA YA FIFA CONNECT & TMS ILIYOANDALIWA NA TFF


  TIMU sita za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara wakiwemo vigogo, Simba, hazikupeleka wawakilishi kwenye Semina ya mafunzo ya kujikumbusha matumizi ya mfumo wa Usajili na Uhamisho wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), maarufu kama FIFA Connect &TMS.
  Mbali na Simba SC, timu nyingine za Ligi Kuu ambazo hazikuwa na wawakilishi kwenye mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kufanyika leo Jijini Dar es Salaam ni Singida Fountain Gate, Kitayosce, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar na Coastal Unión.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAPUUZIA SEMINA YA FIFA CONNECT & TMS ILIYOANDALIWA NA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top