• HABARI MPYA

  Sunday, July 23, 2023

  SIMBA SC YAMTAMBULISHA KIPA MPYA KUTOKA BRAZIL


  KLABU ya Simba imemtambulisha mlinda mlango Jefferson Luis Szerban de Oliveira Junior kutoka Resende ya kwao, Brazil kuwa mchezaji wake mpya kuelekea msimu ujao.
  Jefferson Luis Szerban de Oliveira Junior anakwenda kuwa kipa wa nne kwenye kikosi cha Simba baada ya Aishi Manula, Ally Salum na Ally Ferouz.
  Kwa ujumla anakuwa mchezaji mpya wa 10 mpya kwenye kikosi cha Simba wakiwemo Wacameroon wawili, beki wa katí Che Fondoh Malone Junior kutoka Cotton Sport ya kwao na kiungo mshambuliaji, Leandre Essomba Willy Onana kutoka Rayon Sport ya Rwanda.
  Wengine wapya Simba ni kiungo Mkongo Fabrice Luamba Ngoma kutoka Al Hilal ya Sudan, mawinga José Luis Miquissone kutoka Al Ahly ya Misri na Aubin Kramo Kouamé kutoka ASEC Mimosas ya kwao, Ivory Coast.
  Kuna wazawa wanne ambao beki wa kulia, David Kameta ‘Duchu’ kutoka Mtibwa Sugar, beki wa katí, Hussein Kazi kutoka klabu ya Geita Gold, kiungo Abdallah Hamisi Riziki kutoka Orapa United FC ya Botswana na mshambuliaji wa zamani wa Azam FC Shaaban Iddi Chilunda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAMTAMBULISHA KIPA MPYA KUTOKA BRAZIL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top