• HABARI MPYA

    Sunday, July 30, 2023

    TANZANIA YAWACHAPA ZANZIBAR 1-0 MICHUANO YA CECAFA WASICHANA U18


    BAO pekee la Aisha Mnunka limeipa Tanzania ushindi wa 1-0 dhidi ya Zanzibar katika mchezo wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa mabinti chini ya umri wa miaka 18 leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
    Ushindi huo wa tatu baada ya Tanzania kuzifunga Burundi na Ethiopia unaiweka kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kuelekea mechi ya mwisho na Uganda.
    Mechi nyingine ya leo Ethiopia imeichapa Burundi 2-0 hapo hapo Azam Complex.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TANZANIA YAWACHAPA ZANZIBAR 1-0 MICHUANO YA CECAFA WASICHANA U18 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top