• HABARI MPYA

  Friday, July 14, 2023

  KMC YAACHA TISA NA KUSAJILI WANANE WAPYA


  KLABU ya KMC imeachana na wacheza tisa baada ya kumaliza mikataba yao na kusajili wengine nane kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
  Hao ni Matheo Antony, Nurdin Balora, David Kisu, Mohamed Samata, Frank Zakaria ,Issac Kachwele, Kelvin Kijili, Steve Nzigamasabo na Ally Ramadhan.
  Wachezaji wapya nane ni Wilbol Maseke, Rahimu Shomary, Fredy Tangalo, Vincent Abubakar, Andrew Simchimba, Juma Shemvuni, Rodges Gabriel na Twalib Mohamed.
  Aidha, KMC ambayo msimu ujao itakuwa chini ya kocha Mmarekani mzaliwa wa Somalia, Abdulhamid Moalin inatarajiwa kuingia kambini kesho kuanza maandalizi ya msimu mpya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC YAACHA TISA NA KUSAJILI WANANE WAPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top