• HABARI MPYA

    Friday, July 28, 2023

    PAMBANO LA NGUMI LA KIMATAIFA LIVE TV 3 KESHO


    MABONDIA pambano la Bongo Fighting Championship (BFC) wakamilisha zoezi la Kupima uzito na Afya zao huku bondia wakike nchini Tanzania afunguka mazito mara baada ya kukutana Uso kwa uso na Mpinzani wake Homakoma. 
    Zoez hilo la kupima uzito limefanyika mapema leo Julai 28,2023 katika ukumbi wa Superdome Masaki Jijini Dar es salaam na mabondia mbalimbali kujitokeza kwa zoezi hilo la uthibitisho wa awali kabla ya kupanda ulingoni ambapo Muasisi wa pambano hilo  Scott Farrel amepima uzito kuelekea pambano la kirafiki dhidi ya mpinzani wake  Marcus Warry,Abdul ubaya dhidi ya Ivan Maguma wakati Musa dragon dhidi ya Amos kutoka Kenya wakati  Ajemi amani dhidi Khamis msondo, Huku pambano la Muhaythai pambano kuu ni Emmanuel shija dhidi ya Yusuph Fundi a.k.a Jet Lee.
    Aidha,Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa amesema wamejipanga kurusha maudhui yote yatakayojiri katika pambano hilo ambapo ameongeza kuwa mengi mazuri yanakuja mwezi septemba huku akihaidi kuwa Kampuni haitaacha sehemu itagusa jamii kwa maudhui mbalimbali huku akisema kwenye Masumbwi ndio wameingia rasmi burudani zitapamba moto.
    "Bongo fighting championship ni pambano lenye lengo la dhati na wazi kutoa ushirikiano kwa mabondia ambao ni wachanga na wanatokea mitaani pamoja wakongwe kutumia platform ya Startimes ndani ya Tv3 kuonekana mwanzo mwisho kwa maudhui yote na kipekee watashuhudia Pambano la Mwanamke Feriche Mashauri dhidi ya Chiedza Homakoma kutoka Zimbabwe ."
    Kwa upande wake Feriche Mashauri amesema ameshukuru kwa kufika salama mpinzani wake Homakoma kutokana na tatizo kubwa linaloukumba mchezo wa Masumbwi kutofika kwa wapinzani nchi husika ya pambano kwa kusingizia changamoto ya usafiri.
    Hata hivyo amesema amejiandaa vizuri kumkabili mpinzani wake huku akificha kumpiga Ko raundi ya ngapi akiwaacha mashabiki kushuhudia mchezo huo kupitia tv3 au kufika ukumbi wa Superdome Masaki Jijini Dar es salaam. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PAMBANO LA NGUMI LA KIMATAIFA LIVE TV 3 KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top