• HABARI MPYA

  Tuesday, July 18, 2023

  MIQUISSONE NA AL AHLY NDOA YAVUNJIKA RASMI


  KLABU ya Ahly imevunja mkataba na winga wa Kimataifa wa Msumbiji, Luís Jose Miquissone baada ya miaka miwili tangu imsajili kwa mkataba wa miaka minne kutoka Simba SC ya Dar es Salaam.
  Baada ya kutua Al Ahly, Miquissone hakufanikiwa kuendeleza makali yake aliyokuwa nayo Simba na kufika Septemba 2, mwaka jana akatolewa kwa mkopo Abha ya Saudi Arabia.
  Akiwa Abha mambo hayakumuendea vizuri Miquissone, kwani katika kipindi chote cha msimu amecheza mechi nne na hajafanikiwa kufunga hata bao moja na kwa sasa anahusishwa na taarifa za kurejea Simba SC.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MIQUISSONE NA AL AHLY NDOA YAVUNJIKA RASMI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top