KLABU ya Yanga imemtambulisha winga wa kushoto, Mahlatse Skudu Makudubela kuwa mchezaji wake mpya wa tano kuelekea msimu ujao akitokea Marumo Gallants ya kwao, Afrika Kusini.
Wachezaji wengine wapya Yanga mabeki Nickson Kibabage kutoka Singida Fountain Gate, Kouassi Attohoula Yao kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Gift Freddy kutoka SC Villa ya kwao, Uganda na viungo ni Maxi Mpia Nzengeli kutoka AS Maniema Union ya kwao, DRC na Jonás Mkude kutoka Simba SC.
0 comments:
Post a Comment