• HABARI MPYA

  Monday, July 24, 2023

  KIBU DENNIS AFUNGA SIMBA YATOA SARE 1-1 UTURUKI


  KLABU ya Simba SC imetoa sare ya kufungana bao 1-1 na Zira FK ya  Azerbaijan katika mchezo wake wa kwanza wa kujipima kwenye kambi yake ya kujiandaa na msimu mpya mjini Ankara nchini Uturuki.
  Bao la Simba SC inayofundishwa na Kocha Mbrazil, Robert Oliveira ‘Robertinho’ limefungwa na kiungo mshambuliaji, Kibu Dennis Prosper dakika ya 33 huku la Zira FK limefungwa na kiungo Rustam Alamovych Akhmedzade anayecheza kwa mkopo kutoka Qarabağ dakika ya 63.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIBU DENNIS AFUNGA SIMBA YATOA SARE 1-1 UTURUKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top