• HABARI MPYA

  Thursday, July 13, 2023

  TAIFA STARS YAPANGWA KUNDI GUMU KUFUZU KOMBE KA DUNIA 2026


  TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania imepangwa Kundi E pamoja na Morocco, Zambia, Kongo, Niger na Eritrea katika mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Dunia zitakazoandaliwa kwa pamoja na Canada, Mexico na Marekani.
  Kundi A kuna; Misri, Burkina Faso, Guinea-Bissau, Sierra Leone, Ethiopia na Djibouti.
  Kundi B; Senegal, DRC, Mauritania, Togo, Sudan na Sudan Kusini.
  Kundi C; Nigeria, Afrika Kusini, Benin, Zimbabwe, Rwanda na Lesotho.
  Kundi D; Cameroon, Cape Verde, Angola, Libya, Eswatini na Mauritius.
  Kundi E; Tanzania, Morocco, Zambia, Kongo, Niger na Eritrea.
  Kundi F; Ivory Coast, Gabon, Kenya, Gambia, Burundi na Shelisheli.
  Kundi G; Algeria, Guinea, Uganda, Msumbiji, Botswana na Somalia.
  Kundi H; Tunisia, Equatorial Guinea, Namibia, Malawi, Liberia na São Tomé & Príncipe.
  Kundi I; Mali, Ghana, Madagascar, Jamhuri ya Afrika ya Katí, Comoro na Chad.
  Washindi wa makundi hayo yote tisa watajikatia moja kwa tiketi za Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026.
  Washindi wa pili Bora wanne watamenyana katika michuano mdogo na kinara atakamilisha idadi ya timu 10 zitakazoiwakilisha Afrika kwenye Kombe lijalo la Dunia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YAPANGWA KUNDI GUMU KUFUZU KOMBE KA DUNIA 2026 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top