• HABARI MPYA

  Monday, July 24, 2023

  SIMBA SC YAMUUZA SAKHO TIMU YA LIGUE 2 UFARANSA  KLABU ya Simba SC imefikia makubaliano na klabu ya 
  Union Sportive Quevillaise-Rouen Métropole ya nchini Ufaransa kumnunua mchezaji wake, Msenegal Pape Ousmane Pape Ousmane Sakho.
  Winga huyo wa kushoto mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na Simba SC Agosti mwaka 2021 akitokea Teungueth FC ya kwao, Senegal na baada ya misimu miwili mizuri anaondoka Msimbazi.
  Union Sportive Quevillaise-Rouen Métropole, inayofahamika zaidi kama US Quevilly-Rouen, ama US Quevilly, au QRM ni timu inayoshiriki Ligi ya pili kwa ukubwa nchini Ufaransa, Ligue 2.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAMUUZA SAKHO TIMU YA LIGUE 2 UFARANSA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top