• HABARI MPYA

  Thursday, July 20, 2023

  SIMBA SC YASAJILI BEKI WA KATI WA GEITA GOLD


  KLABU ya Simba SC imeendelea kujiimarisha kwa kumsajili beki wa katí, Hussein Kazi kutoka klabu ya Geita Gold inayoshiriki pia Ligi Kuu ya NBC ya Tanzania Bara.
  Huyo anakuwa mchezaji mpya wa nne mzawa baada ya David Kameta ‘Duchu’ kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, kiungo Mtanzania, Abdallah Hamisi Riziki kutoka Orapa United FC ya Botswana na mshambuliaji Shaaban Iddi Chilunda aliyewahi kutamba Azam FC kabla ya kupelekwa kwa mkopo Tenerife ya Hispania.
  Kwa ujumla Simba SC imesajili wachezaji wapya nane hadi sasa, wengine wanne ni wa kigeni wakiwemo Wacameroon wawili, beki wa katí Che Fondoh Malone Junior kutoka Cotton Sport ya kwao na kiungo mshambuliaji, Leandre Essomba Willy Onana kutoka Rayon Sport ya Rwanda.
  Wachezaji wengine wapya Simba ni kiungo Mkongo Fabrice Luamba Ngoma kutoka Al Hilal ya Sudan, winga wa kushoto na Aubin Kramo Kouamé kutoka ASEC Mimosas ya kwao, Ivory Coast.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YASAJILI BEKI WA KATI WA GEITA GOLD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top