• HABARI MPYA

    Wednesday, July 26, 2023

    AZAM FC YACHAPWA 3-1 NA STADE TUNISIEN MECHI YA KIRAFIKI LEO TUNISIA


    TIMU ya Azam FC imechapwa mabao 3-1 na Stade Tunisian katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Pac Hedi Enneifer mjini Bardo nchini Tunisia.
    Hata hivyo, mchezo huo haukumalizika baada ya Kocha wa Azam FC Youssoupha Dabo kuamuru vijana wake watoke nje dakika ya 62 kutokana na kutoridhishwa na uchezeshaji wa refa na vitendo visivyo vya kiungwana vya wapinzani.
    Beki wa kushoto wa Azam FC, Edward Charles Manyama alikimbizwa hospitali baada ya kuumizwa mkono na mchezaji wa Stade Tunisien.
    Bao pekee la Azam FC iliyoweka kambi mjini Sousse nchini Tunisia kujiandaa na msimu mpya limefungwa na mshambuliaji wake tegemeo, Mzimbabwe Prince Dube Mpumelelo dakika ya 53.
    Huo ni mchezo wa pili Azam FC wanafungwa kati ya minne waliyocheza baada ya awali kufungwa 3-0 na Esperance huku wao wakishinda mechi mbili, 3-0 dhidi ya Al Hilal ya Sudan na 2-1 dhidi ya wenyeji wengine, US Monastir.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YACHAPWA 3-1 NA STADE TUNISIEN MECHI YA KIRAFIKI LEO TUNISIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top