• HABARI MPYA

  Friday, July 21, 2023

  SHIJA NA FUNDI KUZIPIGA MUAY THAI LIVE TV3 JULAI 29


  KAMPUNI ya Bongo Boxing Fighting (BFC) imeandaa mapambano 14 ya ngumi aina ya Muay Thai (Ngumi za Thai) yatakayochezwa Julai 29, mwaka huu Superdom Masaki, Dar es Salaam.                          
  Pambano hilo lirushwa moja kwa moja ( live) kupitia chanal ya Tv3 kampuni ya Star Times Tanzania.      
  Mkurugenzi wa Masoko wa Startimes Media, David Malisa alisema wameshirikiana na BFC kuendeleza mchezo huo na mingine ijayo ikiwemo kickboxing ili kuendelea kuinua vipaji vya wachezaji wa mchezo huo.
  Alisema: "Wengi waliokuwa wateja wetu walitamani kuona mchezo wa ngumi, niwaambie wakae mkao wa kula, Jumamosi ijayo itakuwa ‘live’ kupitia chanel yetu ya Tv3 itaonesha pambano hilo
  Promota wa mapambano hayo ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa The Superdome, Scott Patrick alisema Dar es Salaam juzi kuwa kutakuwa na pambano kuu litakalomshirikisha bondia Abdul Ubaya dhidi ya bondia kutoka Uganda Ivan Mgumba watakaowania Mkanda wa Dunia wa WBC.
   na mengine yajayo naamini mtafurahia."
  Mabondia wengine watakaopanda ulingoni ni Emanuel Shija dhidi ya Yusuph Fundi, Mbaraka Mtange dhidi ya Paul Owen, Abdulrazaki Kazumari dhidi ya Emanuel Patrick, Mwingereza Tomiwa Akindele dhidi ya Johnson Kihegula, Imani Matendo dhidi ya Frank Epimaki na wengine.
  Pia, Musa Said dhidi ya Mkenya Amos Lion, mwandaaji wa ngumi hizo, Scott Farrel dhidi ya Marcus Warry, Fariche Joseph dhidi ya Mzimbabwe, Chiedza Homakoma na Hamis Msondo dhidi ya Ajemi Amani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SHIJA NA FUNDI KUZIPIGA MUAY THAI LIVE TV3 JULAI 29 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top