• HABARI MPYA

  Saturday, July 29, 2023

  YANGA YASAJILI MSHAMBULIAJI MPYA KUTOKA GHANA  KLABU ya Yanga imemtambulisha mshambuliaji Hafiz Wontah Konkoni (23) kutoka Bechem United ya kwao, Ghana kuwa mchezaji wake mpya kuelekea msimu ujao.
  Huyo anakuwa mchezaji mpya wa nane baada ya mabeki Nickson Kibabage kutoka Singida Fountain Gate, Gift Freddy kutoka SC Villa ya Uganda, Kouassi Attohoula Yao, viungo, Peodoh Pacôme Zouzoua wote kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast.
  Wengine ni viungo Jonás Mkude kutoka Simba SC, Mahlatse Skudu Makudubela kutoka Marumo Gallants ya Afrika Kusini na Maxi Mpia Nzengeli kutoka AS Maniema Union ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YASAJILI MSHAMBULIAJI MPYA KUTOKA GHANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top