• HABARI MPYA

  Sunday, July 16, 2023

  WAZIRI AWATUNUKU VYETI WAHITIMU 106 CHUO CHA MICHEZO


  WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dkt. Pindi Chana jana aliwatunuku vyeti wahitimu 106 wa Stashahada katika Chuo Cha Michezo Malya kilichopo wilayani Kwimba Mwanza.
  Waziri Pindi Chana amewapongeza wahitimu hao ambapo amewataka kutumia elimu waliyoipata katika chuo hicho kuendeleza vipaji katika maeneo yao na shule wanazofundisha ili vijana wengi wa Kitanzania wapate fursa za ajira kupitia michezo.
  "Wizara yangu, Elimu Sayansi na Teknolojia, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na Ofisi ya Rais-TAMISEMI tumejipanga kuondoa changamoto ya muundo wa Utumishi kwa wahitimu wa chuo hiki", amesema Waziri Pindi Chana.
  Ameongeza kuwa, Serikali katika mwaka ulioshia Juni 30, 2023 imeshatoa kiasi cha shilingi 1.699,156.17 kwa ajili ya maendeleo ya ujenzi wa Hosteli ya chuo hicho pamoja na shilingi 291,030,542.49 kwa ajili hatua za awali za ujenzi wa Akademia ya michezo ndani ya chuo hicho.
  Wahitimu hao wamehitimu katika kozi ya Uongozi  wa Michezo, Elimu ya ufundishaji michezo  pamoja na elimu ya mazoezi ya viungo katika michezo.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAZIRI AWATUNUKU VYETI WAHITIMU 106 CHUO CHA MICHEZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top