• HABARI MPYA

  Thursday, July 20, 2023

  KOPUNOVIC ALIYEWAHI KUINOA SIMBA SC ATUA TABORA UNITED


  ALIYEWAHI kuwa kocha wa Simba SC, Mserbia Goran Kopunovic amejiunga na klabu ya Tabora United ya Tabora iliyopanda Ligi Kuu ya NBC kama Kitayosce FC.
  Goran Kopunovic (56) ni kocha mwenye uzoefu aliyeanzia kwenye kucheza kama mshambuliaji nyumbani kwao, Serbia kabla ya kuja Afrika ambako amefundisha timu za Polisi ya Rwanda katí ya 2010 na 2013 na Simba SC ya Dar es Salaam mwaka 2015.
  Baada ya hapo alirejea kwao, Serbia kabla ya kwenda Hungary kufundisha timu ya BFC Siófok katí ya 2015 na 2017 na Salavan ya Urusi hadi mwaka jana na sasa anarejea Tanzania kwa awamu ya pili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOPUNOVIC ALIYEWAHI KUINOA SIMBA SC ATUA TABORA UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top