• HABARI MPYA

  Wednesday, July 19, 2023

  YANGA SC YASAJILI NYOTA MWINGINE WA ASEC MIMOSAS


  KLABU ya Yanga imemtambulisha kiungo Peodoh Pacôme Zouzoua (26) kutoka ASEC Mimosas ya kwao, Ivory Coast kuwa mchezaji wake mpya wa saba kuelekea msimu ujao.
  Peodoh Pacôme Zouzoua aliyesaini mkataba wa miaka miwili anakuwa mchezaji wa tano wa kigeni mpya Yanga baada ya mabeki,
   beki Kouassi Attohoula Yao kutoka ASEC Mimosas pia, Gift Freddy kutoka SC Villa ya kwao, Uganda mawinga Mahlatse Skudu Makudubela kutoka Marumo Gallants ya kwao, Afrika Kusini na Maxi Mpia Nzengeli kutoka AS Maniema Union ya kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Wachezaji wengine wapya Yanga SC ni wazawa, beki Nickson Kibabage kutoka Singida Fountain Gate na kiungo Jonás Mkude kutoka kwa mahasimu, Simba SC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YASAJILI NYOTA MWINGINE WA ASEC MIMOSAS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top