• HABARI MPYA

  Thursday, July 20, 2023

  SIMBA SC YAMSAJILI SHAABAN IDDI CHILUNDA ALIYEWAHI KUWIKA AZAM FC


  KLABU ya Simba imemtambulisha mshambuliaji aliyewahi kutamba Azam FC kabla ya kwenda Tenerife ya Hispania, Shaaban Iddi Chilunda kuwa mchezaji wake mpya wa sita kuelekea msimu ujao. 
  Wachezaji wengine wapya Simba SC ni beki wa kulia mzawa, David Kameta ‘Duchu’ kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, beki wa katí Che Fondoh Malone Junior kutoka Cotton Sport ya kwao, Cameroon, kiungo wa ulinzi, Mkongo Fabrice Luamba Ngoma kutoka Al Hilal ya Sudan, winga wa kushoto, Aubin Kramo Kouamé kutoka ASEC Mimosas ya kwao, Ivory Coast na mshambuliaji Mcameroon, Leandre Essomba Willy Onana kutoka Rayon Sport ya Rwanda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAMSAJILI SHAABAN IDDI CHILUNDA ALIYEWAHI KUWIKA AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top