• HABARI MPYA

  Saturday, July 22, 2023

  MAYELE, BANGALA NA DJUMA SHABANI KWAHERI YANGA SC


  NYOTA watatu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), beki Djuma Shabani, kiungo Yanick Bangala na Fiston Kalala Mayele historia yao imefungwa Yanga baada ya misimu miwili.
  Wachezaji hao na beki Mmali, Mamadou Doumbia hawajatambulishwa kama sehemu ya kikosi cha Yanga cha msimu mpya kwenye Siku ya Mwananchi jioni hii klabu hiyo ikimenyana na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mayele anahusishwa na kuhamia Pyramids ya Misri, wakati Djuma Shabani na Bangala wanaweza kurejea klabu za kwao, TP Mazembe ya Lubumbashi na AS Vita ya Kinshasa.

  Hiki ndio kikosi kizima kipya cha Yanga msimu wa 2023-2024


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE, BANGALA NA DJUMA SHABANI KWAHERI YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top