• HABARI MPYA

  Thursday, July 13, 2023

  YANGA SC YAMTAMBULISHA RASMI FUNDI MAXI MPIA NZENGELI  KLABU ya Yanga imemtambulisha winga Maxi Mpia Nzengeli kutoka AS Maniema Union ya Kindu, jimbo la Maniema, kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwa mchezaji wake mpya wa nne kuelekea msimu mpya.
  Maxi Mpia Nzengeli ambaye amechezea timu ya taifa ya DRC kwenye michuano ya CHAN, anakuwa mchezaji mpya wa nne Yanga baada ya mabeki Nickson Kibabage kutoka Singida Fountain Gate, Gift Freddy kutoka SC Villa ya kwao, Uganda na kiungo Jonás Mkude kutoka Simba SC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAMTAMBULISHA RASMI FUNDI MAXI MPIA NZENGELI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top