• HABARI MPYA

  Thursday, May 18, 2023

  USM ALGER WATINGA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA


  TIMU ya USM Alger imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast usiku wa Jumatano Uwanja wa 
  Julai 5, 1962 Jijini Algiers.
  Mabao ya USM Alger yamefungwa na washambuliaji wazawa, Khaled Bovusseliou dakika ya 28 na Abdelfetah Ismaïl Belkacemi dakika ya 80.
  Sasa USM Alger watakutana na Yanga iliyoitoa Marumo Gallants ya Afrika Kusini, ikishinda 2-0 nyumbani na 2-1 ugenini.
  Mechi ya Kwanza ya Fainali itachezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam Mei 28 na marudiano Juni 3 Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: USM ALGER WATINGA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top