• HABARI MPYA

  Saturday, May 20, 2023

  FIRMINO AINUSURU LIVERPOOL NA KIPIGO ANFIELD


  WENYEJI, Liverpool wameambulia sare ya kufungana bao 1-1 na Aston Villa katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield, Liverpool.
  Jacob Ramsey alianza kuifungia Aston Villa dakika ya 27, kabla ya Roberto Firmino kuisawazisha Liverpool dakika ya 89.
  Liverpool wanafikisha pointi 66 katika mchezo wa 37, ingawa wanabaki nafasi ya tano wakizidiwa pointi tatu na Manchester United ambao pia wana mechi moja mkononi, wakati Aston Villa inafikisha pointi 58 za mechi 37 nafasi ya saba.
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FIRMINO AINUSURU LIVERPOOL NA KIPIGO ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top