• HABARI MPYA

  Wednesday, May 17, 2023

  INTER MILÁN YATINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA


  TIMU ya Inter Milan imefanikiwa kwenda Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya mahasimu, AC Milan usiku wa Jumanne Uwanja wa Giuseppe Meazza Jijini Milan nchini Italia.
  Bao hilo pekee limefungwa na Lautaro Martínez dakika ya 74 akimalizia kazi nzuri ya Romelu Lukaku na sasa Inter Milán inakwenda Fainali kwa ushindi wa jumla wa 3-0 kufuatia kuwachapa AC Milan 2-0 kwenye mchezo wa kwanza hapo hapo Giuseppe Meazza wiki iliyopita.
  Inter Milán sasa itamaubiri mshindi wa jumla katí ya Manchester City na Real Madrid zinazomenyana usiku wa Jumatano Uwanja wa Etihad Jijini Manchester baada ya sare ya 1-1 kwenye mechi ya kwanza wiki iliyopita Uwanja wa Santiago Bernabeu Jijini Madrid.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: INTER MILÁN YATINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top