• HABARI MPYA

  Sunday, May 21, 2023

  MAN CITY WAICHAPA CHELSEA 1-0 KUSTAWISHA UBINGWA WAO


  BAO pekee la Julian Alvarez dakika ya 12 limeipa Manchester City ushindi wa 1-0 dhidi ya Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Ushindi huo unawafanya Manchester City wazidi kuustawisha ubingwa wao wa tatu mfululizo, wakifikisha pointi 88 katika mchezo wa 36, mbele ya Arsenal wenye pointi 81 za mechi 37.
  Kwa upande wao Chelsea wamebaki na pointi zao 43 za mechi zao 36 nafasi ya 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY WAICHAPA CHELSEA 1-0 KUSTAWISHA UBINGWA WAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top